banner

MKUU

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

ERASTO SIMA Mkuu Wa Wilaya Korogwe

Korogwe TC | Korogwe DC

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ni kati ya Halmashauri tisa katika Mkoa wa Tanga; na ipo kati ya  latitudo 40 15’ kusini na 5015’ kusini mwa ikweta na longitudo 380 0’ mashariki na 38 045’ mashariki.mwa greenwich ikiwa na eneo la kilomita za mraba 3,544, sawa na asilimia 12.9 ya eneo la Mkoa wa Tanga ambalo ni kilomita za mraba 27,348.

Kiutawala ina Tarafa nne za Mombo, Bungu, Magoma na sehemu ya Tarafa ya Korogwe, Kata 20 na vijiji 122 pamoja na Vitongoji 610. Kati ya Kata hizo Kata ya Mombo ni Mamlaka ya Mji Mdogo kuanzia mwaka 2005 na ina Vitongoji 20.
Idadi ya wakazi kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 kwa mwaka 2010 Halmashauri  inakadiriwa kuwa 254,215 wakiwemo wanaume 125,402 na wanawake 128,813, ambapo ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka ni asilimia 1.93.

DIRA, DHAMIRA NA MALENGO YA HALMASHAURI:

3.1 DIRA: “Kuona kwamba watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe wamepata maisha bora na kujenga uchumi imara na wao wenyewe wameelimika na kupata huduma bora za msingi na kufanya maamuzi kwa misingi ya utawala bora na demokrasia ifikapo mwaka 2015”.

3.2 DHAMIRA: “Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe imedhamiria kutoa huduma bora za msingi, kujenga jamii iliyoelimika, uchumi imara unaohimili ushindani na kutoa maamuzi kwa misingi ya utawala bora ili kupunguza umaskini ifikapo mwaka 2015”.

3.4 MALENGO: Ili kutekeleza dhamira na dira yake. Halmashauri inayo malengo makuu saba yafuatayo:

Huduma imeboreshwa na maambukizi ya VVU/UKIMWI yamepungua.

 

Utawala bora, uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika kuleta ufanisi na umakini katika kutoa huduma vimeboreshwa na kuimarika.

Huduma za kijamii katika sekta za Afya, Maji, Elimu, Utamaduni na Vijana zimeboreshwa.

 

Matumizi endelevu ya maliasili yanayozingatia utunzaji wa mazingira na matumizi bora ya ardhi yameimarishwa.

Kipato cha jamii, uhakika wa chakula, shughuli za kiuchumi, kilimo, mifugo, biashara, ushirika na vikundi vya uzalishaji mali vimeimarika na kuongezeka.

 

Miundombinu ya kiuchumi na kijamii imeboreshwa na kuimarika.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

.