Mkinga

-
Wilaya ya Mkinga ni mojawapo ya Wilaya nane za Mkoa wa Tanga ambayo ilianzishwa rasmi tarehe 01/07/2006 baada ya kugawanywa toka Wilaya ya Muheza ambayo ilianzishwa mwaka 1974. Wilaya hii imepakana na Wilaya ya Muheza na Tanga kwa upande wa kusini, Wilaya ya Lushoto na Korogwe upande wa magharibi, Jamhuri ya Kenya upande wa kaskazini na Bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki.
Wilaya ya Mkinga imegawanyika katika kanda kuu tatu kutokana na tofauti ya kiwango cha mvua. Kanda hizo ni: Ukanda wa nyanda za Juu, ukanda wa kati na ukanda wa Pwani.
Anuani:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga,
S.L.P 6005,
TANGA.
Simu: +255 272645631
Fax : +255 272645632
Email: dedmkinga@yahoo.com
:-
RASHID NDALE Mkuu wa Wilaya Mkinga
