| Uongozi |

Dr Mhando
Mganga Mkuu wa Mkoa -Tanga |
|
Hospitali ya Mkoa ipo chini ya Katibu Tawala mkoa ambayo inaendeshwa kwa usimamizi wa Mganga Mkuu wa Mkoa.
Mganga Mkuu wa Mkoa ni Dr Muhando
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Bomb Dr Mtatifikolo
Mkoa wa Tanga unajumla ya Zahanati , Vituo vya Afya ambavyo vina uwezo wa kuchukua vitanda , kwa sasa kuna vitanda xx,
aidha mkoa una Hospitali xx zenye uwezo wa kuchukua vitanda na vitanda vilivyopo ni xx |
|
|
|
| Utangulizi |
Mkoa wa Tanga una hospitali 11 (Hospitali 5 za Serikali zenye jumla ya vitanda 1,204 na 6 binafsi na mashirika ya dini zenye vitanda 404). Vituo vya afya vilivyopo ni 34 na zahanati 246 (Serikali 197 na binafsi 49). Hospitali moja inatoa huduma kwa wastani wa watu wapatao 193,556 ikilinganishwa na lengo la taifa la watu 100,000. Kituo cha afya kimoja kinahudumia wastani wa watu wapatao 83,815 wakati lengo la taifa ni watu 50,000 kwa kituo na zahanati moja inatoa huduma kwa wastani wa watu 9,000 wakati lengo la taifa ni watu 10,000. |
| |
| Huduma za Akina Mama na Watoto |
Hadi sasa Mkoa wa Tanga haujafanikiwa vya kutosha katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto chini ya miaka 5. Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja ni 100/1000 (taifa 96/1000) na watoto chini ya miaka 5 ni 162/1000. Hii ina maana kwamba watoto wengi wanafariki kabla ya kufikia umri wa miaka 5. Hali hii imepunguza umri wa kuishi hadi miaka 47 kwa wanaume na 49 kwa wanawake ikilinganishwa na wastani wa miaka 50 ya umri wa kuishi kitaifa. Vifo vya akina mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi vimeshuka toka 280/100,000 mwaka 2004 hadi 202/100,000 mwaka 2006.
Watoto chini ya miaka (5) hupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile Surua, Pepopunda na Polio n.k. Kwa mwaka 2006 mafanikio ya chanjo yalikuwa: Polio 95.8%, Surua 98.9%, BCG 88.6%, DPT3 94.7%, TT2 87.8% na Vitamin A 95.8%.
Ili kuinua kiwango cha utoaji huduma za afya, Bodi za afya zimeundwa katika Jiji la Tanga na Halmashauri ya Lushoto, Korogwe, Handeni na Pangani. Mifuko ya kununulia dawa (Drug Revolving Fund) imeanzishwa katika hospitali za Serikali; na utaratibu wa uchangiaji huduma (Cost sharing) umeanzishwa katika hospitali ya Mkoa, hospitali za Wilaya na baadhi ya vituo vya afya na zahanati hususani katika wilaya za Tanga na Lushoto. Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) imeanzishwa kwenye Wilaya za Pangani, Muheza, Handeni na Lushoto. Huduma za afya zinaendelea kuboreshwa kwa msaada wa Mfuko wa Huduma za Afya (Health Basket Fund). Elimu ya afya itaendelea kusisitizwa ili watu wajikinge na maradhi ya kuambukiza hasa malaria, UKIMWI, Kipindupindu, tauni na uti wa mgongo.
Aidha ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF) ulidhibitiwa kwa chanjo ya mifugo na elimu kwa umma baada ya mgonjwa mmoja kufariki katika wilaya ya Mkinga mwezi February, 2007. |
Jina la Wilaya |
Kasi ya Vifo vya Watoto < 1 |
Kasi ya Vifo vya watoto < 5 |
Kasi ya Vifo vya Akina Mama wajawazito |
Lushoto |
|
3.8/1,000 |
86/100,000 |
Handeni |
|
3.5/1,000 |
183/100,000 |
Pangani |
|
3/1,000 |
250/100,000 |
Korogwe |
|
2.9/1,000 |
222/100,000 |
Muheza |
|
4.4/1,000 |
455/100,000 |
Tanga |
|
3.8/1,000 |
284/100,000 |
Kilindi |
|
4.2/1,000 |
13/100,000 |
Mkoa wa Tanga |
|
3.6 |
202/100,000 |
|
| |
| RASILIMALI ZA AFYA KATIKA MKOA WA TANGA KIWILAYA |
| |
Wilaya |
Zahanati |
Vituo vya Afya |
Hospitali |
Idadi |
Uwezo vitanda |
Vitanda vilivyopo |
Idadi |
VitandaUwezo |
Vitanda Vilivyopo |
Lushoto |
43 |
7 |
225 |
100 |
2 |
225 |
100 |
Handeni |
26 |
3 |
128 |
72 |
2 |
128 |
72 |
Pangani |
13 |
1 |
32 |
18 |
1 |
32 |
18 |
Korogwe |
45 |
4 |
128 |
119 |
2 |
128 |
119 |
Muheza |
59 |
6 |
160 |
148 |
1 |
160 |
148 |
Tanga |
43 |
6 |
160 |
115 |
3 |
160 |
115 |
Kilindi |
19 |
3 |
96 |
73 |
0 |
96 |
73 |
Mkoa wa Tanga |
248 |
30 |
929 |
645 |
11 |
929 |
645 |
|
| |
Programu ya Ukarabati wa vituo vya kutolea huduma ya Afya Mkoani (HIDP) |
|
Mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa kiasi cha Euro 5 millioni. Mradi unahusu ukarabati wa majengo, mifumo ya maji, na umeme na ununuzi wa vifaa katika hospitali ya Bombo, hospitali za Wilaya (isipokuwa Kilindi na Mkinga) na vituo vya afya. Kamati maalum inasimamia utekelezaji wa mradi ngazi ya Mkoa na kila Wilaya. Shughuli za mradi zilianza mwezi Septemba 2005 na zinategemewa kukamilika ifikapo mwezi Juni 2008.
|
| |
Mapambano dhidi ya UKIMWI |
Mkoa unapambana na tatizo la UKIMWI kwa kushirikisha taasisi za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kijamii (CBOs/NGOs), taasisi za dini (FBOs), sekta binafsi na wananchi kwa jumla. Kazi kubwa zilizofanyika ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii mijini na vijijini na kwenye makundi mbalimbali- wafanyakazi, wanafunzi, vijana n.k., kuanzisha na kueneza vituo vya kupima virusi vya UKIMWI, kuimarisha kamati za UKIMWI ngazi zote hadi vijijini n.k. Pia Halmashauri na asasi mbalimbali zinasaidia watoto yatima na wanaokabiliwa na mazingira magumu kutokana na tatizo la UKIMWI
Kampeni ya Kupima Virusi vya UKIMWI kwa hiari, iliyoanza Mkoani mwanzoni mwa Septemba 2007 hadi tarehe 30 Aprili 2008 ilikuwa na mafanikio kutokana na kufikia asilimia 101 ya walengwa. Katika Kampeni hiyo kiwango cha maambukizi kilionekana kuwa asilimia 3.9 (ikiwa 3.0 miongoni mwa Wanaume na asilimia 4.6 kwa Wanawake). Wastani wa Kitaifa ni asilimia 5 |
|
| |
Mpango Maalum wa Afya ya Msingi (MMAM): |
Ili kufikia malengo ya kuwa na zahanati kila kijiji, kituo cha Afya kwenye kila Kata na Hospitali ya Serikali moja kwa kila Wilaya, Mkoa (pamoja na Halmashauri na wadau wengine) utahitajika kujenga Hospitali 3 (Kilindi, Tanga na Mkinga). Vituo vya Afya 123 na zahanati 440.
Ili kutimiza lengo la kuwa na miundombinu ya huduma hizo, fedha zitakazohitajika ni kama ifuatavyo:
- Ujenzi wa zahanati 440 - sh. Bilioni 14.75
- Ujenzi wa vituo vya afya 123- sh. Bilioni 30.75
- Ujenzi wa Hospitali 3 - sh. Bilioni 6.00
Jumla sh. Bilioni 51.50
Ili Mkoa ujitosheleze kutoa huduma za tiba na kinga kwenye maeneo yote ya Serikali za Mitaa, watumishi wa kada mbalimbali wanahitajika. Kiwango cha upungufu wa watumishi wa Afya kwa Mkoa kufikia hadi Juni 2008 ni kama ilivyo kwenye jewali lifuatalo: |
| |
HALI YA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA HADI JUNI 2008 |
KADA |
MAHITAJI |
WALIOPO |
UPUNGUFU |
Madaktari |
22 |
6 |
16 |
Madaktari Wasaidizi |
93 |
52 |
41 |
Madaktari wa Meno |
8 |
0 |
8 |
Matabibu |
558 |
288 |
270 |
Maafisa Wauguzi |
149 |
66 |
83 |
Wakunga |
844 |
270 |
574 |
Wataalamu wa Maabara |
25 |
7 |
18 |
Wafamasia |
8 |
0 |
8 |
Wazoeza Viungo |
8 |
0 |
8 |
Wataalamu wa X - ray |
8 |
0 |
8 |
Maafisa Afya |
140 |
69 |
71 |
Makatibu wa Afya |
16 |
5 |
9 |
Wahudumu wa Afya |
565 |
471 |
94 |
|
| |
CHANGAMOTO KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA NA UFUMBUZI |
- 1. Wilaya za Tanga, Mkinga na Kilindi hazina hospitali za Wilaya. Serikali inaombwa kutoa kipaumbele kwenye kutoa fedha za kutosha kuwezesha ujenzi wa hospitali katika wilaya hizo.
- Mkoa una jumla ya zahanati 246 badala ya 716 zinazohitajika. Wananchi wataendelea kuhimizwa kuanzisha na kuendeleza ujenzi wa zahanati kwenye kila kijiji. Serikali kupitia Serikali za Mitaa itaunga mkono juhudi za wananchi.
- Kuna Uhaba mkubwa wa wataalam wa Afya wa kada mbalimbali ambao unaarithi ubora wa huduma zinazotolewa. Wizara ya Afya na TAMISEMI wanaombwa kusaidia katika kupatikana kwa Wataalam na Watumishi wengine wa Afya ili kuongeza ubora na ufanisi wa utoaji wa Huduma za Afya Mkoani.
- Uhaba wa vitendea kazi mbalimbali kama vile ukosefu wa magari ya wagonjwa kwa Hospitali ya Mkoa na wilaya zote. TAMISEMI isaidie upatikanaji wa magari ya kubebea wagonjwa kwenye kila wilaya na Hospitali ya Mkoa.
- Timu ya usimamizi ya shughuli za Afya ya Mkoa (RHMT) kutotambulika rasmi katika mfumo wa Tawala za Mikoa (Sekretarieti) na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Tunapendekeza timu ya Usimamizi wa Huduma ya Afya Mkoa (RHMT) watambuliwe rasmi na TAMISEMI ili wawe sehemu ya Sekretarieti ya Mkoa kuimarisha usimamizi wa Huduma za Afya Mkoani.
- Uhaba wa nyumba za watumishi wa Afya kuanzia ngazi ya mkoa mpaka vijijini ni tatizo kubwa. Tatizo limeongezeka baada ya Serikali kuwauzia watumishi nyumba zilizokuwa kwenye viwanja vya hospitali hususani wilaya ya Lushoto ambako nyumba kumi (10) zilizoko kwenye eneo la hospitali kuuziwa watumishi (sawa na kuuza hospitali ya Wilaya). Tunashauri Serikali itengue mauzo ya nyumba kama hizo nchini kote.
|
| |
| Wahisani waliopo Mkoani Tanga |
| |
|
Mhisani |
Mradi/Shuhuli |
1 |
TGPSH |
-HIV/AIDS
-Reproductive Health
-CHF
-District support and Quality Management
-Capacity building to health staff
-Public Private partneship |
2 |
Care,World Vision |
Hati Punguzo,Sanitation, HIV/AIDS, Malaria |
3 |
AXIOS |
OVC and VCT |
4 |
MEA |
-VHW-training
-First aids drugs and material |
5 |
PONTESBURY MUHEZA LINK |
-VHW-training
-Rehabilitation and construction of health facilities |
6 |
DCI |
-Capacity Building
-Construction of Health Facilities
-Rehabilitation of Health facilities |
7 |
NACP |
HBC(Home Based Care for people living with HIV/AIDS. |
8 |
HELLEN KELLER |
Rehabilitative servises.Eye care |
9 |
NIMR-NFLP |
Elimination of Elephantiasis/Filariasis and worms infestation in the community |
10 |
Equal Opportunity for All (E0FA) |
Care of disabled |
11 |
NATIONAL VOUCHER SCHEME |
Control of malaria in pregnant mothers and children under five years |
12 |
SHIA-Isnashir |
H/F Rehabilitation |
13 |
KONOIKE |
H/F Rehabilitation |
14 |
UMATI |
Improve access to U MATI intergrated sexual and reproductive health(SRH) services
Youth-10 to 24 years adults |
15 |
APOC |
Control of Onchoceasis |
16 |
Belgium Government |
HBC activities |
17 |
NLFEP |
Lymphatic Filariasis Elimination |
18 |
KODEPA |
-Offer laboratory services
-Pharmacy services
-Health center services |
19 |
Tanga Aids Working Group |
-Couselling of patients,ARVs distribution,HBC activities |
20 |
GLOBAL FUND |
HIV/AIDS prevention through VCT |
21 |
PSI |
Social marketing condom,Safeguard and bednets |
22 |
RFA |
Support CSOs,CBOs on HIV/AIDS |
23 |
PATHFINDERS |
Home based care services |
|
| |
|