JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
tanga
 
     
 
     
ARDHI, UPIMAJI NA RAMANI
 
Ardhi, Upimaji na Ramani [ Nyumbani ] au
 

ARDHI

 
Mr Ardhi
Mshauri wa Ardhi
Sekretarieti ya Mkoa
Contacts ??
Bonyeza hapa >> wizara ya ardhi
 
 
Utangulizi
 
Kufuatana na sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1999 ambayo inahimiza upatikanaji wa viwanja vya kutosha kwa ajili ya  matumizi mbalimbali ,msukumo wa upatikanaji wa viwanja vya matumizi mbalimbali  mkoa unatekeleza
 
Malengo ya Mkoa Sekta ya Ardhi

Katika sekta ya Ardhi malengo makuu ya Mkoa katika kuendeleza Sekta ya Ardhi kipindi cha 2005 – 2010 ni kuhakikisha kuwa

Maeneo yote ya vijiji yanapimwa na kutambuliwa kisheria, kila kijiji kuwa na mpango wa matumizi Bora ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya vijiji inaeleweka vizuri kwa wananchi. 

Kuharakisha upimaji wa mashamba kwa kufuata Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya Mwaka 1999 na upimaji wa viwanja mijini ili kuzuia ujenzi holela. 

Mkoa unatilia mkazo suala zima la kutenga maeneo ya Uwekezaji ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Tanga ni wa pili Kitaifa katika mpango wa utekelezaji wa "Economic Processing Zone- EPZ".  Utekelezaji wa majukumu hayo katika kipindi cha mwaka 2005/06 na mwaka 2007/08 ni kama ifuatavyo

 

Utekelezaji wa Malengo Haya

 
Upimaji wa mipaka ya vijiji, viwanja na mashamba
 
 
  • Vijiji 592 vimepimwa mipaka yake katika Mkoa wa Tanga chini ya Mradi ulioendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mwaka wa fedha 2007/08, hivyo kufanya vijiji vyote 720 kupimwa mipaka yake katika Mkoa wa Tanga.
  • Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi Juni, 2008 vijiji 13 vilipatiwa vyeti vya vijiji katika Wilaya ya Handeni na vijiji 20 katika Wilaya ya Korogwe.
  • Hati za kumiliki ardhi za kimila 20 zimetayarishwa katika Wilaya ya Korogwe na 1,100 katika Wilaya ya Handeni.
  • Jumla ya viwanja 3,089 vimepimwa sawa na asilimia 70 ya lengo la kupima viwanja 4,784 katika kipindi cha mwaka 2005/2010.  Jumla ya Hekta 79,122 za mashamba zimepimwa sawa na asililmia 170 ya lengo la kupima hekta 46,650.
 
   
Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi  
Utayarishaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwa vijiji 24 umefanyika.  Aidha, Hati miliki za mashamba 705 zimetolewa katika kipindi cha mwaka 2005 hadi Juni 2008 katika Wilaya ya Handeni chini ya Mradi wa MKURABITA.  
   
Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi  
Jumla ya migogoro 901 inayohusu ardhi iliwasilishwa katika Tume ya Rais ya Kuchunguza Migogoro ya Ardhi.  Jumla ya migogoro 797 imeshatatuliwa, sawa na (88.45%) ya migogoro iliyokuwa imewasilishwa  
   
Baraza la Ardhi na Nyumba  

Katika jitihada za Serikali za kutatua migogoro ya ardhi nchini Mabaraza ya Ardhi yameundwa katika Kata na Vijiji mbalimbali.  Aidha, Mabaraza ya Ardhi na Nyumba yameundwa katika Miji.  Katika Mkoa wa Tanga Baraza la Ardhi na Nyumba limeanzishwa katika Jiji la Tanga mwaka 2004.

Katika Baraza hilo jumla ya migogoro 868 ilifunguliwa kati ya mwaka 2004 hadi Juni, 2008.  Migogoro 662 sawa na 76.27% ilikwisha tatuliwa na iliyobaki ni 206
 
   
Maeneo ya Uwekezaji  
Katika utekelezaji wa agizo la kutenga maeneo ya kanda maalum za uwekezaji, maeneo yafuatayo yametengwa katika Jiji la Tanga  
  • Ndumi/Mwambani – hekta 25 zimepimwa kwa ajili ya viwanda. (Barabara ya Tanga – Pangani).  Katika eneo hilo Hekta 82 zimeongezwa kwa ajili ya upanuzi wa eneo la Bandari.  Gharama zilizokisiwa kwa ajili ya uthamini, upangaji pamoja na upimaji wa eneo hilo ni shs. 37,835,000/=.  Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Port Authority – TPA) imeshatoa idhini Halmashauri ya Jiji kulipwa fedha hizo kwa kazi hiyo.
  • Neema Special Economic Zone – Hekta 1,000.  Imekadiriwa kuwa Jiji litahitaji jumla ya Shs. 930,000,000/= kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.  Fedha hizi zitagharimia uthamini wa mali, utayarishaji wa michoro ya Mipango Miji, upimaji wa ardhi, usimamizi wa ardhi, Utengenezaji wa miundombinu kama barabara, maji, umeme n.k.
  • Golf Industrial Area – Viwanja 15 vimepimwa.
  • Kange Industrial Area – Eka 50 (hekta 20).  Eneo hili liliombwa na NDC na kufanyiwa upimaji, kwa sasa matayarisho ya ujenzi wa “Industrial Park” yanaendelea.
  • Amboni Sisal Properties Ltd (eneo la Pongwe), jumla ya eka 275 (hekta 110) zimetengwa kwa ajili ya Uwekezaji.
 
   

MAENEO YA ARDHI YALIYOTENGWA KWA AJILI YA UWEKEZAJI

 
   

WILAYA

SHUGHULI

ENEO (HEKTA) ZILIZOPO

Muheza

Kilimo

2,300

Pangani

Kilimo

3,000

Korogwe Mji

Kilimo cha Umwagiliaji

1,730

Korogwe Wilaya

Kilimo
Ufugaji
Ujenzi wa kiwanda cha Saruji
Ujenzi wa Hoteli
Elimu na ujenzi wa majengo ya afya

19,286
2,000
20
6

85

Lushoto

Kilimo cha matunda

10,000

Handeni

Kilimo cha matunda na mboga
Ufugaji wa ng’ombe na kondoo
Kilimo cha Mpira

8,400

3,500
1,500

Kilindi

Kilimo cha mboga
Ufugaji wa ng’ombe

1,829
400

Tanga

Viwanda, bandari, majengo ya biashara n.k.

1,300

 
   
   
       
 
Ardhi, Upimaji na Ramani [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Box 5095 Tanga, TEL: 027 - 2642430, FAX: 027-2647752