JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
tanga
 
     
 
     
BARABARA NA MAWASILIANO
 
Barabara [ Mawasiliano ] [ Nyumbani ] au
 
 
BARABARA:
 

Mkoa una jumla ya barabara zenye urefu wa km 5,623 ambazo ziko chini ya Wakala wa barabara yaani TANROADS na Halmashauri.

TANROADS inahudumia barabara Kuu na za Mkoa zenye jumla ya urefu wa Km 1,528. ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo: 

  • Barabara kuu za lami zina urefu wa Km. 268
  • Barabara kuu za changarawe zina urefu wa Km. 58
  • Barabara za Mkoa za lami Km. 38
  • Barabara za Mkoa zisizo za lami Km. 1,093

Halmashauri za Mkoa wa Tanga zina mtandao wa barabara zenye urefu wa Km 4,095 ambazo zimegawanyika kwenye makundi ya barabara za Wilaya za Mjini na barabara za vijijini.

Katika sekta hii lengo ni kuhakikisha kuwa barabara zote zinapitika kwa urahisi wakati wote wa mwaka. 
 
Miradi ya Barabara Mkoa wa Tanga
 

Miradi mikubwa ya Ujenzi wa barabara mkoani Tanga ni kama ifuatavyo

  1. Baraba ya Tanga – Horohoro (65 Km) imekwishafanyiwa usanifu wa kina na itajengwa kwa kiwango cha lami chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekani (Millenium Challenge Corporation).
  2. Barabara ya Tanga – Pangani – Saadani – Bagamoyo (178 Km).  Barabara hii inafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.  Kazi inaendelea na itakamilika mnamo tarehe 30 Aprili, 2009.
  3. Barabara ya Mkata – Handeni (54 Km) na Korogwe – Handeni – Mziha (140 Km).  Barabara hizi zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami, kazi inaendelea na itakamilika.  Kazi yote itakamilika mnamo mwezi Oktoba, 2008.
Miradi mikubwa ya Ukarabati wa barabara Mkoani Tanga
  1. Barabara ya Manga – Segera – Tanga (160 Km) itafanyiwa ukarabati wa kuiimarisha kwa kuwekewa tabaka jipya la lami na kuipanua sehemu za milima ili kuongeza usalama kwa watumiaji.  Mradi huu unafadhiliwa na DANIDA na tayari awamu ya kwanza kuanzia Chalinze – Kitumbi (125 Km) imeshapata Mkandarasi.  Kazi zitachukua muda wa miezi 30 kukamilika kwa gharama ya shilingi 42.6 bilioni.  Awamu ya Pili toka Kitumbi – Tanga (113 Km) zabuni zinategemewa kutangazwa mwezi Julai  2008.
  2. Barabara ya Segera – Korogwe – Mkomazi (108 Km), nayo iko katika mpango wa kuifanyia ukarabati wa kuiwekea tabaka jipya la lami ili kuiimarisha chini ya mkopo toka Benki ya Dunia
 
 
Barabara zilizo chini ya Halmashauri  
   

Halmashauri inatekeleza miradi ya barabara kupitia fedha za mfuko wa barabara (Road fund), fedha za Mpango wa Usafiri wa Serikali za Mitaa (LGTP) na fedha za Mpango wa Uendelezaji wa Mazao ya Kilimo na Masoko (AMSDP).

 
   
Matengenezo ya barabara za Halmashauri  
    Matengenezo yanayofanyiwa Barabara zilizochini ya Halmashauri ni.
    1. Matengenezo ya kawaida (Routine maintenance) km 14.2
    2. Matengenezo ya sehemu korofi (Spot Improvement) km 26.2
    3. Matengenezo maalum (Periodic maintenance) km 9.1
 
   
   
 
         
 
Barabara [ Majengo ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Box 5095 Tanga, TEL: 027 - 2642430, FAX: 027-2647752