| |
| Mkoa wa Tanga unahuduma zote za mawasiliano ikiwa ni; Huduma za bandari, Huduma za Reli, Huduma za Simu za mikononi, Huduma za Posta, Huduma za Televisheni, Huduma za Umeme na Huduma za Redio |
Redio
| |
Mamlaka ya Bandari |
| |
Mwaka 2005/2006 Bandari ya Tanga ilihudumia mizigo ya tani 395,206 (au asilimia 79 ya uwezo). Katika kipindi cha 2006/07 Bandari ililenga kuhudumia jumla ya tani 520,375. Utekelezaji ulikuwa ni tani 516,922 sawa na asilimia 99.3 ya lengo.
- Meli zilizoingia bandari ya Tanga ziliongezeka kwa asilimia 15.12 kutoka meli 271 mwaka 2005/06 hadi meli 312 mwaka 2006/2007.
- Kutokana na ukarabati na upanuzi wa eneo pamoja na kuboresha vifaa/zana za kazi n.k. bandari ya Tanga imeongeza uwezo wake wa kuhudumia mizigo kutoka tani 500,000 mwaka 2005 hadi tani 700,000 mwaka 2008.
- Mipango iliyopo ni pamoja kuendelea kununua vitendea kazi kutoa mafunzo kwa wafanyakazi na ujenzi wa bandari mpya Mwambani (Tanga).
|
| |
| Huduma za reli (Railway Services) |
Reli ya Tanga ina umri wa mika 100 tangu ilipoanzishwa. Mwaka 2007 baada ya Shirika kubinafsishwa Mwekezaji mpya Tanzania Railways Limited katika mkataba wake wa utoaji huduma hapa nchini alisitisha utoaji huduma katika reli ya Tanga.
Mkoa unaishukuru Serikali kwa jitihada iliyofanyika ya kurudisha huduma ya usafiri wa reli Tanga; ambapo uzinduzi ulifanyika rasmi tarehe 13/6/2008 kwa usafirishaji wa mizigo kutoka Tanga kwenda Mwanza na Kigoma. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na uongozi wa TRL, huduma hiyo itatolewa mara mbili kwa wiki. |
| |
| Huduma za Posta |
Huduma za posta zipo katika wilaya zote nane za mkoa wa Tanga; Tanga, Korogwe, Handeni, Pangani, Mkinga, Lushoto, Muheza na Kilindi. Kilindi ofisi ndogo ya Shirika la Posta imefunguliwa katika mji mdogo wa Songe; Makao Makuu ya Wilaya ya Kilindi.
Huduma inazotoa Posta ni pamoja na ..... |
| |
| Huduma za Simu |
Makampuni yanayotoa huduma za simu mkoani ni makampuni matano (5) yaani TTCL, CELTEL, VODACOM na TIGO na ZANTEL
Mkoa una mawasiliano ya simu za mkononi katika Wilaya zote 8. Kwa upande wa Kampuni ya simu TTCL Mkoa wa Tanga mapato kimkoa yamepanda kwa asilimia 90% ikilinganishwa na mwaka 2005. Huduma zimeboreka hadi kufikia asilimia 85% baada ya Kampuni kujenga mtambo wa mawasiliano ya simu za Mkononi CDMA na mtambo wa simu za mezani aina ya MSAN. Aidha, upanuzi wa mtambo aina ya MEGAPLEX na mtambo wa WLL (SIWAYA) umefanyika ili kuboresha mawasiliano.
Kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi Juni, 2008 Kampuni ya Simu TTCL imeweza kutekeleza jumla ya Miradi 12 yenye uwezo (capacity) wa njia 3,176 na hivyo kufanya ongezeko la Miradi 5 kwa asilimia 200%.
Kati ya 2005 hadi 2007/08, wateja wa TTCL wanaotumia simu za kawaida na simu za mkononi (Mobile) wameongezeka kutoka 6,053 mwaka 2005 hadi wateja 8,667 mwaka 2007/08. (Ongezeko la asilimia 43 (43%). Pia wateja wa huduma ya mtandao (Data/Internet) (kupitia TTCL wameongezeka kutoka 20 mwaka 2005 hadi 92 mwaka 2007/08. (Ongezeko la asilimia 360 |
| |
Televisheni |
| |
Mkoa unapata mawasiliano kwa njia ya televisheni kupitia vituo vya TBC 1, ITV, Star TV, BSTV na Tanga Television (TaTV). Tanga Television ilianzishwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga mwaka 2005. |
| |
| Redio |
| Mkoa unapata mawasiliano kwa njia ya Redio zifuatazo: TBC (Taifa), TBC (FM), Redio One na Sauti ya Injili Moshi. Aidha, Mkoa ulifanya uzinduzi wa kituo cha Clouds FM mwezi Septemba, 2006. Pia vituo vingine viwili vya Radio (F.M. station) vimeanzishwa katika Jiji la Tanga mwaka 2007. (Radio Mwambao FM na Radio Huruma) |
| |
| HUDUMA YA UMEME |
| |
Mkoa una vituo vitatu vya usambazaji umeme. Vituo hivyo ni:
1. Majani Mapana Tanga - 33/11kV (2x10MVA)
2. Wilaya ya Lushoto - 33/11kV (1x5MVA)
3. Wilaya ya Korogwe - 22/11kV (1x1.5MV
Miji yote ya Makao Makuu ya Wilaya ina huduma za umeme wa “Grid” isipokuwa Wilaya ya Kilindi. Wapimaji (surveyors) wanaendelea na upimaji wa njia ya kupita nyaya za umeme kwenda Songe. Umeme umeshafika eneo la Kwediboma ambapo tayari wananchi wananufaika na huduma hiyo.
Ili kupeleka umeme hadi Songe, Serikali kupitia wakala wa Nishati vijijini (Rural Energy Agency – REA) imetenga shs. 1.5684 billioni kwa ajili ya kutekeleza mradi huo hadi Songe. Vijiji vya njiani (mkabala na laini ya umeme) pia vitapatiwa huduma hiyo. Mradi utatekelezwa katika awamu mbili na utahusisha vijiji vya Mgera, Kibirashi, Mafisa, Majengo, Vilindwa, Bokwa, Kwastemba na Nkama.
Kuhusu Wilaya mpya ya Mkinga, mradi wa kupeleka umeme Makao Makuu ya Wilaya (Kasera) umekamilika kwa asilimia 50. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, nyumba ya Mkuu wa Wilaya na nyumba za watumishi zilizojengwa zimewekwa umeme. Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mwaka 2008/09 imetenga shs. 88 Millioni kwa ajili ya kusambaza umeme maeneo yaliyo jirani na Makao Makuu ya Wilaya. |
| |
| |
| |
|