JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
tanga
 
     
 
     
VIWANDA NA BIASHARA
 
Biashara [ Nyumbani ] au
 
UTANGULIZI
 

Mkoa wa Tanga ulikuwa kati ya Mikoa yenye viwanda vingi vikimilikiwa na sekta binafsi kabla na baada ya uhuru. Uzalishaji wa mazao ya biashara hasa katani, kahawa na chai na kuendelea kwa viwanda, kuliufanya Mkoa wa Tanga kushika nafasi ya pili kimaendeleo baada ya Dar es Salaam

 
Idadi ya viwanda na Uzalishaji

Mkoa una jumla ya viwanda 36 (Viwanda vikubwa na vya kati).  Mwaka 2006 uzalishaji ulikuwa tani 980,543. Viwanda viliuza bidhaa ndani ya nchi kwa jumla ya  tani 750,279 zenye thamani ya Sh. 134,683,242,383.  Vile vile mauzo ya bidhaa nje ya nchi yalifikia tani 205,859 zenye thamani ya dola za Marekani 11,840,802.  Bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni zile za nyuzi (yarn); nyuzi za mkonge; kamba za mkonge; saruji, Chai vipodozi; sabuni za unga (Foma); minofu ya samaki na bidhaa za mbao.

Mwaka 2007, uzalishaji viwandani ulifikia tani 1,051,470.  Bidhaa kiasi cha tani 774,201.4 zenye thamani ya Sh. 192.4 billioni ziliuzwa ndani ya nchi na mauzo ya nchi za nje yalifikia tani 622,097 zenye thamani ya Dola za Marekani 2,503,990,126.

 
Vituo vya Habari kwa wafanyabiashara Mkoa wa Tanga

Mkoa umeanzisha kituo cha kutoa habari za biashara kwa wafanyabiashara wadogo mjini Tanga (Tangamano Business Information Centre)

Mkoa una matawi ya Chama cha Wafanyabiashara na Wakulima (Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture) katika jiji la Tanga na miji mikuu ya Wilaya za Korogwe, Muheza na Lushoto.

Tarehe 21.12.2006 Baraza la Biashara la Mkoa lilizinduliwa likiwa na madhumuni ya kubuni njia za kuboresha uchumi mkoani; kuhamasisha uwekezaji na kusuluhisha migogoro ya kibiashara.  Kadhalika, Mkoa umetenga maeneo huru ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi (EPZ & SEZ).  Maeneo yaliyotengwa ni eneo la viwanda Kange na eneo la Ndumi, Gofu, Neema na Pongwe katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.

 
BARAZA LA BIASHARA LA MKOA (REGIONAL BUSINESS COUNCIL)
 

Tarehe 21.12.2006 Baraza la Biashara la Mkoa lilizinduliwa likiwa na madhumuni ya

  • Kubuni njia za kuboresha uchumi mkoani;
  • Kuhamasisha uwekezaji na
  • Kusuluhisha migogoro ya kibiashara. 

Ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Mkoa, zimeundwa kamati (Working committees) 5 nazo ni:-

  1. Kamati ya Kilimo na usindikaji wa bidhaa (Agriculture and Agro-processing Committee)
  2. Miundombinu (Infrastructure)
  3. Uwekezaji (Investment Committee)
  4. Uboreshaji wa Mazingira ya ufanyaji Biashara (Business Environment)
  5. Ulinzi na Usalama (Security Committee)

Mkoa umetenga maeneo huru ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi (EPZ & SEZ).  Maeneo yaliyotengwa ni eneo la viwanda Kange na eneo la Ndumi, Gofu, Neema na Pongwe katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.

 
    Idadi ya Viwanda vya Umma
 
Viwanda vya Umma hadi mwaka 1995 vilikuwa 12.  Navyo ni
    1. Tanga Cement Co. Ltd  - Utengenezaji wa saruji
    2. Tembo Chipboards Co - Mkumbara – Utengenezaji wa bidhaa za mbao
    3. Tanga Steel Rolling Mills – Utengenezaji wa nondo na misumari
    4. Tanga Dairies Co. Ltd – Maziwa
    5. Sabuni Detergents Industries – Foma
    6. Sikh Saw Mills – Utengenezaji bidhaa za mbao
    7. Tanzania Fertilizer Co. Ltd – Utengenezaji wa mbolea
    8. Tangold Co. Ltd – Korogwe – Usindikaji wa matunda
    9. Giraffe Wattle Extract Co. – Lushoto - Miwati
    10. Tanzania Cordage Ltd (Ngomeni Tanga) – Kamba za katani
    11. East Usambara Tea Co. – Amani   Muheza – Usindikaji wa chai.
    12. Mkata Saw Mills – Utengenezaji wa bidhaa za mbao.
 

UBINAFSISHAJI

 
Hadi kufikia mwaka 2006 viwanda vyote vilivyokuwa vya UMMA vilikuwa vimebinafsishwa;  na baadhi  vimebadilishiwa majina; navyo ni

JINA LA ZAMANI                     JINA LA SASA

  1. Tanga Steel Rolling Mills      →      Unique Steel Rolling Mills
  2. Tanga Dairies                      →      International Food Processors (Azania)
  3. Sabuni Detergents Industries    →      Sabuni Products Ltd – SPL
  4. Sikh Saw Mills             →       Ply & Panel (T) Ltd
  5. Tanzania Fertilizer Co.        →    GBP (Matumizi ya Kiwanda yamebadilishwa kuwa hifadhi ya matufa ya nishati)
  6. Mkata Saw Mills                  →      Anisha Saw Mills (Hakijawahi kufanya kazi)
  7. Giraffe Wattle Extract Co.      →      Lushoto Lion Wattle Co. Ltd
  8. Tanzania Cordage Ltd (Ngomeni Kamba)                   →      TANCORD (1998) Ltd
 
    Viwanda vya Sekta Binafsi

Mwaka 1995 kulikuwa na viwanda binafsi ambavyo ni:-

  1. Tanganyika Industries Corporation (TIC) – Uzalishaji wa kamba za katani (kimekwisha kufungwa).
  2. Amboni Plastics – Uzalishaji wa bidhaa za plastiki (kimekwisha kufungwa).
  3. Kilimanjaro Blankets Corporation Ltd – Uzalishaji wa blanketi
  4. TIP Soap – Uzalishaji wa sabuni aina ya Mbuni na Gadenia (Kwa sasa kinaitwa TIP SOAP (2005) Ltd)
  5. Amboni Spinning Mills – Uzalishaji wa nyuzi/kamba za mkonge
  6. Anjari Soda Factory – Uzalishaji wa vinywaji baridi aina ya “Healtho”.
  7. Simba Lime Factory – Uzalishaji wa chokaa
  8. Bombay Burmah Trading Corp. Ltd – Uzalishaji wa chai
  9. Ambangulu Tea Factory – Uzalishaji wa chai
  10. Kirani Soap Industries – Uzalishaji wa sabuni aina ya MNARA (Kwa sasa kimefungwa).
  11. Dindira Tea Factory – Uzalishaji wa chai
  12. CIC – Uzalishaji wa nguo (Sasa kinaitwa “AFRITEX”)
  13. Quality Products – Uzalishaji wa bidhaa za plastiki (Kilihamishiwa DSM)
  14. PEE PEE (T) Ltd – Uzalishaji wa bidhaa za mifuko
  15. Tanga Fresh (Ushirika wa Wafugaji) – Uzalishaji wa maziwa.
  16. Usambara Spinning Mills – Lugongo – Utengenezaji wa kamba za mkonge.
 
    Viwanda Vipya
Viwanda vipya vya sekta binafsi vimeweza kujengwa katika kipindi cha mwaka 1995 – 2006.  Navyo ni
    1. Pembe Flour Mills – Usagaji wa unga wa ngano
    2. Tanga Pharmaceutical & Plastics Ltd – TPPL – Utengenezaji wa vipodozi
    3. Mamujee Products – Utengenezaji wa vipodozi
    4. ARM (T) Co. Ltd – Uzalishaji wa chokaa
    5. ESRI Enterprises – Uzalishaji wa mifuko ya plastiki (Kimefungwa)
    6. Sea Products Ltd – Usindikaji wa samaki (Pweza)
    7. E.A. Briquettes Co. Ltd – Utengenezaji wa mkaa
    8. Mponde Tea Factory – Usindikaji wa chai (Lushoto)
    9. Natural Choice Co. Ltd – Lushoto – Uzalishaji wa maji na juisi – Soni – Lushoto.
    10. Herkulu Tea Estate – Usindikaji wa chai – Lushoto
    11. KIMSO Saw Mills – Uzalishaji wa mazao ya mbao – Lushoto
 
 
 
         
 
Biashara [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Box 5095 Tanga, TEL: 027 - 2642430, FAX: 027-2647752