ELIMU |
| |
| Elimu Mkoa wa Tanga unasimamia elimu ya awali, elimu ya msingi na elimu yasekondari |
|
| Mkoa unashirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kusimamia na kuendesha shughuli za elimu. Mkoa unatekeleza Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES 2004-2009). na Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM II) baada ya MMEM I Kumaliza muda wake (2002- 2006) |
| |
| |
ELIMU YA AWALI |
Mkoa wa Tanga una jumla ya Shule za awali 483 zikiwemo za madarasa ya Serikali 850 na shule za awali zisizo za Serikali 12. Idadi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hizo ni 30,257 wakiwemo wavulana 16,395 na wasichana 13,862. |
| |
| |
| |
| ELIMU YA MSINGI |
Darasa la kwanza mwaka 2008 mkoa uliandikisha watoto 76,670.
Mkoa wa Tanga una jumla ya Shule za Msingi 920 mwaka 2008, kati ya hizo shule 853 ni za Serikali na 11 ni shule zisizo za Serikali. Wanafunzi wa shule za msingi ni 411,130 kati yao wavulana ni 211593 na wasichana ni 199537.
Mkoa wa Tanga una jumla ya walimu wa shule za Msingi 7017, kati yao 3514 ni wanaume na 3503 ni wanawake |
| |
| IDADI YA SHULE ZA MSINGI KIWILAYA |
| |
Wilaya |
Makadirio ya Idadi ya wa tu 2006 |
Idadi ya shule za msingi |
Wastani wa idadi ya watu kwa shule |
Idadi ya Vijiji /Mitaa |
Wastani wa vijiji/ Mitaa kwa shule |
Pangani |
45,885 |
31 |
1,480 |
33 |
0.9 |
| Muheza |
294,326 |
106 |
|
|
|
Mkinga |
170 |
1,731 |
175 |
1.0 |
Korogwe |
272,956 |
159 |
1,717 |
135 |
1.2 |
Tanga |
261,613 |
91 |
767 |
23 |
4.0 |
Handeni |
280,927 |
142 |
2,103 |
176 |
1.1 |
Kilindi |
165,005 |
99 |
648 |
64 |
1.3 |
Lushoto |
437,379 |
218 |
2,006 |
162 |
1.3 |
Total |
1,758,091 |
880 |
1,638 |
714 |
1.3 |
|
| |
Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) |
| |
MMEM I 2002 - 2006 ni mpango wa maendeleo wa Elimu ya Msingi ambao umejikita katika maeneo makuu |
| |
Mkoa umepata mafanikio makubwa kutokana na utekelezaji wa mpango wa Maendeleo ya elimu ya Msingi (MMEM). Idadi ya shule za Msingi imeongezeka kutoka shule 756 mwaka 2002 hadi shule 920 mwaka 2008.
- Idadi ya vyumba vya madarasa (vya kudumu) imeongezeka kutoka 3,928 mwaka 2002 hadi 7,781 mwaka 2008.
- Nyumba za Waalimu zimeongezeka kutoka 706 mwaka 2002 hadi nyumba 2,490 mwaka 2008.
- Aidha idadi ya Waalimu katika shule za msingi imeongezeka kutoka 6,172 mwaka 2002 hadi Waalimu 8,349 mwaka 2008
|
|
|
TAKWIMU ZA ELIMU YA MSINGI MKOA WA TANGA 2008 |
Aina ya Mahitaji |
Mahitaji |
Yaliyopo/zilizopo/Waliopo |
Upungufu |
Vyumba vya Madarasa |
9,916 |
7,781 |
2,135 |
Nyumba za Walimu |
10,556 |
2,490 |
8,060 |
Waalimu |
10,283 |
8,329 |
1,954 |
Vyoo (matundu) |
20,572 |
8,666 |
11,906 |
Madawati |
181,400 |
139,924 |
41,553 |
|
| |
| MATOKEO YA MTIHANI WA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2005 |
Mwaka 2007 wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa cheti Elimu ya Msingi katika Mkoa wa Tanga walikuwa 41157, wakiwemo Wavulana 20,881 na Wasichana 20,276
Waliofanya mtihani walikuwa 39,760 kati yao Wavulana ni 20,188 na Wasichana ni 19,572 sawa na asilimia 98.2. Jumla ya wanafunzi 1,397 hawakufanya mtihani kati yao Wavulana ni 693 na Wasichana ni 704 . Sababu za kutofanya mtihani ni utoro, mimba, ugonjwa na vifo.
Waliofaulu mtihani walikuwa 25,800 kati yao wavulana ni 14,002 na Wasichana ni 11,798 sawa na asilimia 63.8.
Jumla ya wanafunzi 25,476 wakiwemo wavulana 13,678 na wasichana 11,798 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2008. Idadi hii ni sawa na 98.7% ya watahiniwa wote 25,800 waliofaulu Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) mwaka 2007
Wanafunzi 324 sawa na (1%) ya waliofaulu wamekosa nafasi ya kuendelea na masomo ya Sekondari, kati yao Wavulana324 hakuna Wasichana waliokosa nafasi.
|
|