Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali za Mitaa walikagua miradi katika Halmashauri za Mkoa wa Tanga ambazo ni Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri ya Mji Korogwe, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Mkinga, Muheza, Pangani, Handeni, Kilindi na Lushoto kuanzia tarehe 22 mpaka 24 mwezi Oktoba mwaka 2008.
Wajumbe walitembelea miradi mingi ya jamii ikiwa ni miradi ya Maji chini ya Mpango wa Maji Quick wins, Miradi ya Afya (Health basket Fund), Miradi ya Kilimo (ASDP na PADEP), Miradi ya Elimu (MMES), Miradi ya Programmu ya Kusaidia Halmashauri (LGCDG), Miradi ya Barabara (Road Fund), Miradi ya Maliasili (Participatory Forest Management )Miradi ya Jamii chini ya TASAF na minigine Mingi |
|