JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
tanga
 
     
 
     
UZINDUZI WA TOVUTI ZA MIKOA ...
 
Website [ Nyumbani ] au
 
 
Waziri Mkuu asisitiza Matumizi ya Mtandao - Internet
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa umekuwa katika michango mbalimbali ya kukuza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) katika ngazi ya mkoa na halmashauri za wilaya kwa lengo la kujenga serikali mtandao (e-government). Kuimarika kwa matumizi haya ya (TEKNOHAMA) kutasaidia sana kurahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika shughuli mbalimbali za kila siku kati ya serikali (mkoa), halmashauri za wilaya na wadau wengine.
 

Moja ya vitu ilivyoshughulikia ni uanzishwaji wa Tovuti za Mikoa kwa Mikoa yote ya Tanzania bara. Ambapo tovuti hizi zimezinduliwa rasmi na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda tarehe 19 Februari 2009 halfla hiyo imefanyika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.

Akizungumza katika Hafla hiyo Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda alisema dhana ya upatikanaji wa habari ni haki ya kila raia wa mtanzania, kupata habari, kutafuta na kupokea na kuzitumia yeye anavyotaka.

kwa kupata tovuti za mikoa jukumu mnalotakiwa kulijua ni kuhakikisha kuwa tovuti hizi zinakuwa na habari zote za msingi kila wakati ili kusaidia mwananchi wakati wowote anapotaka kujua habari zote zinazohusu mkoa anaotaka, lazima kuweka taarifa kila wakati "update" kila wakati tunataka sera na mikakati ya utekelezaji wa serikali ipatikane kiurahisi kwa umma s

WAZIRI MKUU
PICHANI : Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. MIZENGO PINDA (aliyekaa kulia) akizindua tovuti za mikoa mkoani Kilimanjaro. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Same(nyuma) , Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mkuu wa wilaya ya Siha, Outcome manager - TAMISEMI, Katibu wa Waziri Mkuu na Mtaalam wa TEKNOHAMA Mkoa wa Kilimanjaro
 

Sasa tumefanya hii kazi sio kwamba temukurupuka tu kufanya kazi hii tumeanza wizarani kwa kuweka vitengo vya habari na tumeweka wasemaji wa kila wizara. nimategemeo yangu kuwa na mikoa inao watu ambao ndio wasemaji wa mkoa ambapo mtu anapotaka kupata habari mnasema muone fulani hapo atapata habari zote
tunataka sera na mikakati ya utekelezaji wa serikali ipatikane kiurahisi kwa umma

Ilani ya Chama cha Mapinduzi imebainihsa umuhimu wa habari na mawasiliano katika kujenga uchumi imara. kwa kupitia maelekezo hayo yanasema katika kujenga uchumi imara kutasaidia kuandaa mazingira mazuri kuhusu masoko, ubora wa viwango kwenye biashara. kwa hiyo na halmashuri nazo mnayo nafasi ya kutangaza halmshauri zenu vivutio vyenu kwenye tovuti hizi. Nasema kuwa kwangu leo hii ni "milestone" nzuri sana. Kwa mikoa ambayo inasuasua ambayo imebakia mikoa 11 lazima TAMISEMI muwasukume waweze kukamilisha kazi hii. Mikoa hakikisheni mnapata taarifa tutapata taarifa zote za fedha, mipango, taarifa za mazingira, kilimo na namna mnavyokabiliana nayo, habari za afya huduma za jamii taarifa nyingi tu zinapatikana kwenye tovuti hizi. hivyo fanyeni matumizi ya tovuti iwe fashion kila ukikaa upende kwenda kwenye tovuti. hili nauzoefu ninapoenda kwenye mikutano mikubwa utaona nchi za wenzetu baada ya mikutano wanakuwa "busy" kwenye "internet" lakini sisi watanzania baada ya kikao mtu anakimbilia kileo akipata anaona dunia yote kafunguliwa yeye.

nampongeza mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro kwa kufanya kazi hii, nenda halmashauri yako moja na nyingine mpaka uzimalize wote kuhakikisha wanaunga mkono suala lako hili.

kwangu hili litanisaidia sana wasaidizi wangu watajua mambo yanayoendelea mikoani. muda wote ntakua na taarifa za Mikoa yangu.

  kusoma Hotuba ya Waziri Mkuu BONYEZA HAPA >>
   
 
         
 
Tovuti [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Box 5095 Tanga, TEL: 027 - 2642430, FAX: 027-2647752