JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
tanga
 
     
 
     
KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA TANGA
 
RCC I 2008 [ Nyumbani ] au
 
Utangulizi
 

Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Paul Amaniel Chikira ambae ni Katibu wa kikao hiki aliwaeleza wajumbe kwamba, hiki ni kikao cha kwanza kwa mwaka 2008/209 ambacho kinafanyika leo tarehe 18 Oktoba, 2008. Aidha alisema kwamba kikao hiki kimehudhuriwa na wajumbe wa kikao wa kisheria 28 kati ya wajumbe 40. 

Mwenyekiti wa Kikao hiki Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mohamed Abdulaziz (Mb) aliwashukuru wajumbe kwa kuhudhuria na kufungua kikao
 
Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mohamed Abdulaziz (Mb) akifuatilia jambo wakati wa Kika
 
Taarifa zilizowasilishwa Katika Kikao
 
  1. TAARIFA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KIPINDI CHA 2007/2008
  2. TAARIFA YA MAENDELEO YA ELIMU YA MSINGI
  3. TAARIFA YA ZIARA YA MHE. MKUU WA MKOA KATIKA KITUO CHA UTAFITI SELIAN ARUSHA
  4. TAARIFA YA TATHMINI YA MWISHO YA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA
  5. TAARIFA FUPI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAPINDUZI YA KILIMO
  6. UJENZI WA SOKO LA KISASA LA MBOGA SEGERA WILAYANI KOROGWE
  7. MRADI WA MACEMP
 
TAARIFA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZWA KIPINDI CHA MWAKA 2007/2008
 
Ukaguzi wa miradi ulifanyika kuanzia tarehe 6-28/11/2008 katika halmashauri zote za Mkoa wa Tanga. Lengo la ukaguzi lilikuwa ni kuona kama utekelezaji wa miradi unaenda sawa na thamani ya miradi husika.Kulikuwa na makundi 4 yaliyohusisha wataalamu kutoka ngazi ya Mkoa na Halmashauri ambayo yalikagua miradi 104 ikiwemo ya Elimu, Afya, mazingira, Maji, Ushirika,biashara na barabara.Katika kila mradi uliokaguliwa wataalamu waliainisha mapungufu na kutoa maoni na ushauri juu ya namna ya kuboresha mradi husika
Ng'ombe Mazinde 2008
 
Lengo la mradi ni kuimarisha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kwa wanakikundi wa kikundi cha wanawake wajane – (KIKUMU) wapatao 30 katika kijiji cha Mazinde Wilayani Korogwe.  Fedha iliyotengwa ni Tsh.18,000,000/= toka TASAF utaratibu unaotumika ni “kopa ng’ombe lipa ng’ombe”.
Wataalamu wa Sekretarieti ya Mkoa na Wataalamu wa Halmashauri wakipata maelezo kutoka kwa Mfugaji wa Ng'ombe wa Maziwa katika kijiji cha Mazinde Wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga. Mwenye Kofia ni Ndugu Gervas P. Msanga ( Katibu Tawala Msaidizi -Huduma za Menejimenti Sekretarieti ya Mkoa) ambaye ndiye kiongozi wa Msafara akifuatana na Mchumi wa Jiji la Tanga Ndugu Moshi aliyeshika Ng'ombe wengine ni Ndugu Juma Mdaki ( Mtaalamu Sekretarieti ya Mkoa) hayupo pichani na Bibi Beatrice - Afisa Mipango (W)- Mkinga
 
majadiliano wajumbe

Wajumbe walitaka kujua juu ya mambo yafuatayo kuhusiana na Taarifa hii ya Ukaguzi wa Miradi

  1. Miradi inayokaguliwa ni ipi? ile inayoendelea tu ama ni pamoja na ile ambayo imeshatengewa fedha?.
  2. Fedha zinazotolewa ni kiasi gani zimetumika?  kiasi gani zimebakia?  ukilingani na asilimia ya kazi iliyofanyika?
  3. Taarifa haijahusisha mambo kama vile upungufu wa wataalamu fedha n.k.
  4. Kamati ikikutana kuna miradi ambayo haijakamilika ama ipo chini ya kiwango ina uwezo wa kusimamisha usiendelee au ina uwezo wa kuchukua hatua gani?
 

MAJIBU

Wakati wa kukagua miradi mambo mengi hujitokeza ikiwepo suala la wataalamu kuishi mbali na hivyo kushindwa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi pale unapohitajika lakini pia wakuu wa Idara zinazohusika kutotoa ushirikiano kwa wataalamu kwa wananchi pale unapohitajika lakini pia wakuu wa Idara zinazohusika kutotoa ushirikiano kwa wataalamu wanaokwenda kukagua miradi hiyo. Miradi inayohusika katika ukaguzi ni ile inayodhaniwa na Serikali Kuu.Miradi inayokaguliwa ni baadhi tu ya miradi na siyo yote bali ukaguzi unaanzia kwenye ngazi ya wilaya hadi vijijini na unazingatia thamani ya mradi husika.
 
 

TAARIFA YA MAENDELEO YA ELIMU YA MSINGI

Wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2008 Mkoa wa Tanga ni 56,446 wanaotarajiwa kufaulu ni 31,652 sawa na asilimia 56.5%. Wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha I mwaka 2009 ni wanafunzi 31,652. Madarasa yanayohitajika ni 791, yaliyopo ni 583 yanayojengwa ni 261. Madawati yanayohitajika ni 31,652 yaliyopo ni 22,741 upungufu ni Madawato 8,911. Vyoo matundu yanayohitajika ni 1,582 yaliyopo 1,273 upungufu 309
 
 
TAARIFA YA ZIARA YA MHE. MKUU WA MKOA KATIKA KITUO CHA UTAFITI SELIAN ARUSHA
 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mohamed Abdulaziz (Mb) alifanya ziara ya mafunzo katika kiituo cha utafiti Seliani Kanda ya Kaskazini tarehe 15-17 Oktoba 2008 na alifuatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Ndugu Paul Amaniel Chikira na Katibu Tawala Msaidizi (Huduma za Uchumi) Ndugu Ndibalema Kisheru na Mshauri wa Kilimo wa Sekretarieti ya Mkoa Ndugu Lameck Tungu.

Madhumuni ya ziara hiyo yalikuwa ni kuona na kujifunza kazi za utafiti wa Kilimo zinazofanyika kituoni hapo, mafanikio na matokeo yake na jinsi ya kunufaika nayo mkoa wa Tanga.

Aidha baada ya kurejea katika ziara hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa aliwaagiza viongozi na watendaji toka Halmashauri zote 9 katika Mkoa wa Tanga (Halmashauri za Wilaya za Handeni, Kilindi, Lushoto, Korogwe, Mkinga, Muheza na Pangani, Halmashauri ya Mji Korogwe na Halmashauri ya Jiji la Tanga) waende Selian Kwa kipindi cha muda wa siku zisizopungua tano (5) ili wakaone na kujifunza yale yote yanayofanyika katika kituo hicho na wakirudi kwenye maeneo yao waweze kuyafikisha yale waliyojifunza kwa walengwa. Aliagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilindi pamoja na wakulima toka Sikimu ya Chajula nao wahudhurie waende kituoni hapo. 

Kuhusu vikundi alisema tayari vimetengwa na vinatarajiwa kuwezeshwa na wataalamu kutoka Seliani, lakini pia Seliani wataleta wataalamu kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga.

 
Majadiliano
 

Mkuu wa Wilaya Kilindi Bibi Sarah Dumba aliwaeleza wajumbe kwamba walitelekeza mara moja maagizo ya Mhe. Mkuu wa Mkoa na kwa kushirikiana na wataalamu waliainisha mafunzo yanayotakiwa kutolewa hivyo wakapeleka wataalamu kwa ajili ya mafunzo ya uzalishaji mbegu za mahindi, maharage, alizeti na viungo.  Na wengine ni kwa ajili ya ukaulishaji wa mbegu bora

Kuhusu vikundi Mkuu wa Wilaya ya Kilindi alisema tayari vimetengwa na vinatarajiwa kuwezeshwa na wataalamu kutoka Seliani, lakini pia Seliani wataleta wataalamu kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga.

 
TAARIFA YA TATHMINI YA MWISHO YA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA
Uzalishaji

Katika mwaka 2007/2008 uzalishaji Mkoa uliweka lengo la kuzalisha chakula kwa Kulima na kutunza jumla ya Hekta. 526,912 za mazao ya chakula ambapo tani 1,210,827 za Mazao ya chakula zilitarajiwa kuvunwa. Mavuno halisi mwaka 2007/08 yalikuwa Tani 866,298 za Mazao ya Chakula

Msimu wa vuli mwaka 2008/2009 mvua za Vuli hazikunyesha vizuri. Mvua zimechelewa kunyesha kwa takribani miezi miwili (2). Hali ya mavuno haitakuwa ya kuridhisha kutokana na kukosekana kwa mvua za vuli

 
Hali ya chakula katika kipindi cha Mwaka 2008/2009
 

Makadirio ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 akilinganisha na mahitaji ya chakula ambapo kwa mwaka mzima Mkoa unahitaji Tani 509,592.  Hivyo kulingana na uzalishaji uliopatikana katika msimu 2007/2008, wa tani 866,298 kumekuwepo na ziada ya chakula ya tani 356, 706 kwaajili ya matumizi katika kipindi cha mwaka 2008/2009.

Kutokana na mvua za vuli kutonyesha vizuri haitegemewi kupatikana mavuno ya kuridhisha hivyo chakula kulichopo kiendelee kutumika kwa uangalifu. Wakulima waepukane na uuzaji holela wa chakula na Wafanyabiashara walanguzi wadhibitiwe na viongozi katika ngazi zote.

 

TAARIFA FUPI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAPINDUZI YA KILIMO

 

Kila Halmashauri iliwasilisha taarifa yake katika utekelezaji wa mpango wa mapinduzi ya kilimo ambao Mpango ulijikita katika maeneo yafuatayo

  1. Uwezeshaji wa wageni katika halmashauri
  2. Mpango wa uuzaji wa mazao kwa stakabadhi/vocha
  3. Mpango wa matumizi ya teknolojia bora katika kilimo (kwa kuzingatia maagizo 4 ya waziri Mkuu)
  4. Mpango wa kuboresha ng’ombe wa kienyeji na kuku wakienyeji na kuongeza tija ya mazao yake.
  5. Maendeleo ya uimarishaji wa ushirika na SACCOS

Katika kuchangia wajumbe walieleza kuwa wananchi wanayo mazao lakini tatizo ni stakabadhi za kununua hayo mazao? Wananchi wameshahamasishwa sana tatizo ni soko la mzao hayo. Pia wajumbe walisisitiza kuwa kata chache zilishirikishwa katika mpango huo na zilizopo ni nyingi ambazo zimeachwa hivyo ufanyike utaratibu wa kuziingiza katika mpango huo na vilevile kuwahamasisha wananchi jinsi ya kuboresha shughuli za vijana katika vikundi. 

 
UJENZI WA SOKO LA KISASA LA MBOGA SEGERA WILAYANI KOROGWE
 

Taarifa ya ujenzi wa soko iliwasilishwa na baadhi ya mambo yaliyojitokeza na Mradi kuwa umechelewa sana toka mpango wake uwekwe. 

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iliahidi kufuatilia suala hili kuona linakwenda kwa haraka zaidi

 
MRADI WA MACEMP

Taarifa ilisomwa na Mkuu wa Idara ya Uchumi.  Alisema kuwa mradi unatakiwa kuwa katika wilaya 305 lakini wilaya zenya sifa ni 196 tu, alisema kuwa miradi inaibuliwa inakwenda katika TASAF, na TASAF inaomba MACEMP.

 
 
RCC [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Box 5095 Tanga, TEL: 027 - 2642430, FAX: 027-2647752