JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
tanga
 
     
 
     
ZIARA YA MH. RAIS MKOANI TANGA 2008
 
Ziara ya Rais Tanga [ Nyumbani ] au
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea mkoa wa Tanga kwa ziara ya Kikazi kwa muda wa siku 10 kuanzia tarehe 14 Julai, 2008 na kumaliza ziara yake tarehe 23 Julai 2008 ambako amepitia wilaya zote nane za mkoa huo kukagua shughuli za maendeleo, kusikiliza kero na faraja ya wananchi, na kuwashukuru wananchi kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi mwaka 2005 kuendelea kuongoza nchi.

Mhe. Rais aliwasili Mkoani akitokea Mkoa wa Morogoro ambapo mkoa ulimpokea wilaya ya Kilindi. Rais alitembelea wilaya zote za Mkoa wa Tanga Handeni, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga, Pangani na Tanga.

Akiwa mkoani Tanga Mhe. Rais alipata fursa ya kuongea na wananchi na kuzindua Jumla ya Miradi 16 Miradi ya kijamii na kiuchumi katika wilaya zote nane za mkoa wa Tanga

 
 
Miradi aliyozindua Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Juni 2008 mkoani Tanga
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika wilaya ya Kilindi alizindua miradi na kuweka Jiwe la Msingi mradi ya umwagiliaji katika kijiji cha Kilindi na mradi wa ujenzi wa Hospitali Teule kijiji cha Miluzi, alifanya mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Miluzi

Wilaya ya Handeni Mhe. Rais alizindua mradi na kuweka jiwe la msingi la Bwawa la Maji kwenjugo Makelele na kuweka jiwe la Ufunguzi wa Masjala ya Ardhi na kukabidhi Hati miliki kijiji cha Mzeri. Mhe. Rais alifanya mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Mzeri

Wilaya ya Korogwe Mhe. Rais alifungua OPD katika Hospitali ya Magunga na kuzindua mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya mkonge kijiji cha Hale. alifanya mkutano wa Hadhara katika kijiji cha mnyuzi

 

Wilaya ya Lushoto Mhe. Rais alifungua Soko la Soni na alifungua OPD ya Hospitali ya Wilaya. alifanya mkutano wa Hadhara katika viwanja vya Saba saba Lushoto mjini

Wilaya ya Mkinga Mhe. Rais alifungua na kukagua majengo ya Makao Makuu ya Wilaya yaliyopo Kasera na kufungua Zahanati ya Vuo. alifanya mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Duga

Wilaya ya Muheza Mhe. Rais  alifungua Sekondari ya Mtindiro na alifungua shule ya Sekondari Muheza -High School. alifanya mkutano wa Hadhara katika uwanja wa mpira kijiji cha Kicheba

Wilaya ya Pangani Mhe. Rais alifungua Shule ya Sekondari Bushiri. alifanya mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Bomani Pangani mjini

Wilaya ya Lushoto Mhe. Rais alifungua Soko la Soni na alifungua OPD ya Hospitali ya Wilaya. alifanya mkutano wa Hadhara katika viwanja vya Saba saba Lushoto mjini

RAIS VUO
Wilaya ya Mkinga Mhe. Rais alifungua na kukagua majengo ya Makao Makuu ya Wilaya yaliyopo Kasera na kufungua Zahanati ya Vuo. alifanya mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Duga
Wilaya ya Muheza Mhe. Rais  alifungua Sekondari ya Mtindiro na alifungua shule ya Sekondari Muheza -High School. alifanya mkutano wa Hadhara katika uwanja wa mpira kijiji cha Kicheba
Wilaya ya Pangani Mhe. Rais alifungua Shule ya Sekondari Bushiri. alifanya mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Bomani Pangani mjini
Wilaya ya Tanga jiji Mhe. Rais alzindua Mradi wa Ufugaji Samaki, aliweka jiwe la msingi Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa uliopo Mwambani na kuzindua mradi wa maji eneo la mgwisha. alifanya mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Mgwisha
Mhe Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika zahanati ya Vuo, iliyoko wilaya mpya ya Mkinga mkoani Tanga, muda mfupi baada ya kuifungua zahanati hiyo. wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua na kuzindua shughuli mbalimbali za maendeleo Julai 2008
 
 
 
Hotuba ya majumuisho ya ziara Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga
 

Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema sekondari zilizoanzishwa kila kata nchini ni fursa ya kihistoria ya kuleta usawa wa kweli miongoni mwa Watanzania. Aidha, amesisitiza kuwa elimu ndiyo itakuwa siri ya kweli ya mageuzi ya jamii ya Tanzania, na hivyo amewataka viongozi kulisimamia kikamilifu suala la elimu na kuhakikisha linafanikiwa, na kwamba elimu hiyo ya sekondari iliyopanuka katika miaka miwili iliyopita, ndiyo itadhibiti mwenendo mzima wa ongezako la watu nchini.

Katika hotuba yake ya karibu saa tatu kwenye ukumbi wa shughuli mbalimbali wa Hoteli ya Mkonge mjini Tanga, Rais Kikwete alieleza kufurahishwa kwake na jitihada zinazofanywa na wananchi wa Tanga chini ya uongozi wao katika kujiletea maendeleo.

Rais aliyetumia muda mwingi kuelezea umuhimu na manufaa ya elimu kwa umoja na usawa wa Watanzania, aliwaambia viongozi hao wa Mkoa wa Tanga: “Itabidi, ndugu zangu, twende shule. Huu ndiyo ukombozi wetu pekee. Sisi wa ukanda wa Pwani tumekuwa tunachezea elimu, na bado tunafanya mchezo, wakati wale waliotutangulia wanaonyesha umakini mkubwa.

Ni lazima tukimbie wakati wenzetu wanatembelea.” Alisisitiza Rais: “Kama mnavyojua, maeneo yale ambayo hayakuwa na Wamisionari ambao walivutiwa na hali ya hewa, hayakuwa na sekondari na yalibakia nyuma kielimu. Hata baada ya uhuru, sekondari zilikuwa maeneo ya mijini tu. Hapakuwapo sekondari kwenye makao makuu ya wilaya, achilia mbali vijijini.

Hali hiyo ilijenga mazingira ya watu fulani kuwa na fursa zaidi, na wengine kukosa nafasi kama hiyo.” Alisema maana kuu ya kujenga sekondari kila kata ni kutoa fursa sawa kwa Watanzania wote, siyo kwa wale tu waliokuwa na bahati ya kuwa na sekondari za Wamisionari. mfano duga ambako wamisionari hawakufika jamii itapata wapi fursa ya kupata elimu?

 

Rais Jakaya Kikwete amesikitishwa na kasi ndogo ya wazazi na walezi wa wilaya ya Pangani mkoani Tanga katika kupeleka shule watoto wao wenye umri wa kwenda shule.

Kutokana na hali hiyo, Rais amewataka wakazi wa wilaya ya Pangani mkoani Tanga kuongeza jitihada za kuhimiza watoto wao ili wawe wanakwenda shule na kupata elimu itakayowasaidia katika kuboresha maisha yao ya baadaye.

``Ndugu zangu, ni lazima sasa tujipange upya ili kuhakikisha watoto wetu wanakwenda shule kwa kasi mpya. Kinyume chake, Pangani na maeneo mengine ya kando mwa Bahari ya Hindi maendeleo yatakuwa yakija polepole,`` akasema.

Akaongeza kuwa maisha ya sasa yanategemea sana elimu, hivyo akasisitiza kuwa kila mzazi au mlezi ahakikishe mtoto wake

anakwenda shule kupata elimu ya msingi na kwa wale watakaofaulu, ni muhimu wakahakikisha kuwa nao wanakwenda darasani bila kukosa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete wanaangalia watoto waliokuwa wanacheza ngoma za utamaduni katika viwanja vya Kacheba wilayani Muheza,Mkoani Tanga.
 

Rais pia aliwataka viongozi wa Mkoa wa Tanga kuanza kuangalia jinsi ya kutatua tatizo la ardhi ambalo limekuwa kilio kikubwa cha maeneo mbalimbali ambayo rais ametembelea. “Ndugu zangu, kila nilipopita kilio ni ardhi, ardhi, tumebanwa, tumebanwa.

Hili ni bomu la kutega. Linaweza kulipuka ovyo na kusababisha madhara makubwa. Hivyo liangalieni hili kwa umakini.”

Rais Kikwete amesema serikali itahakikisha inafanya kila jitihada za kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwekeza kwenye kiwanda cha usindikaji wa matunda wilayani Muheza, kwa lengo la kuwatafutia wakulima wa machungwa soko la uhakika.

Alisema lengo la kujenga kiwanda hicho licha ya kumtafutia soko mkulima, lakini pia itakuza kipato cha wakulima sambamba na kupunguza kiwango kikubwa cha machungwa yanayoharibika mashambani kwa kukosa wanunuzi hasa nyakati za msimu.

“Serikali inaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumemsaidia mkulima kwa kiasi kikubwa kuwa na soko la uhakika sambamba na kukuza kipato chake ambacho hivi sasa kinapotea kutokana na kiasi kikubwa cha matunda kuharibika…nawaahidi kwamba hili tutalitekeleza haraka iwezekanavyo,”.

Miongoni mwa ahadi alizotoa rais wilayani Muheza ni pamoja na kupeleka darubini katika zahanati ya Kijiji cha Kicheba amabyo darubini hii ilitolewa na Naibu Waziri wa Afya Aisha Kigoda kwa Mganga Mkuu wa Hospitali kwenye kikao cha majumuisho, kuchangia sh milioni mbili katika ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Mtindiro, sambamba na kutafuta magari ya wagonjwa katika wilaya zilizokosa huduma hiyo mkoani hapa.

 
 
Ziara ya Rais Kikwete Tanga 2008 [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Box 5095 Tanga, TEL: 027 - 2642430, FAX: 027-2647752