banner

Muheza

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


 

  •   Historia.
    Wilaya ya Muheza ilianza mwaka 1974, ambayo ilimegwa kutoka katika Wilaya ya Tanga nje. Baada ya kugawanywa Wilaya ya Muheza ilikuwa na  Jimbo 1 la Uchaguzi, Tarafa 6 za Muheza, Bwembwera, Amani, Ngomeni, Maramba na Mkinga,Kata 35 na vijiji 174. Mwaka 2008 Wilaya ya Muheza iligawanywa tena na kuwa wilaya mbili. Wilaya ya Muheza ina Jimbo 1 la Uchaguzi, tarafa 4 za Muheza, Bwembwera, Amani na Ngomeni, Kata 33, vijiji 135 na vitongoji 522

    Eneo la Wilaya.
    Wilaya ya Muheza ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 1,974 ambapo kilometa za mraba 1,145 zinafaa kwa kilimo.Kiasi cha 70% ya eneo linalofaa kwa kilimo ndilo linalotumika kwa shughuli za kilimo.

    Muundo wa Halmashauri ya Wilaya.
    Baraza la Madiwani la Halmashauri ndiyo chombo kikuu kinachoamua na kupitisha mikakati juu ya utekelezaji wa shughuli zote za Halmashauri baada ya kupitiwa na Kamati za kudumu za Halmashauri.  Chini ya Baraza la Madiwani la Halmashauri kuna Kamati tatu za kudumu za Halmashauri ambazo ni:-

    • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango,
    • Kamati ya Elimu, Afya na Maji,
    • Kamati ya Ujenzi, Uchumi  na Mazingira.
    • Kamati ya UKIMWI
    • Kamati ya Maadili

    Shughuli zote za kiutendaji katika Halmashauri zinafanywa na watumishi ambao wapo chini ya Mkurugenzi Mtendaji. Wakuu wa Idara na vitengo ambao wote kwa pamoja wanatengeneza Timu ya Menejiment ya Halmashauri (TMH) na wao ndio washauri wakubwa wa Mkurugenzi kiutendaji. Kwa sasa wakuu wa idara wapo kumi na mbili (12) na vitengo vinne (4).  Hii inatokana na utekelezaji wa hatua ya sita ya Uboreshaji wa Serikali za Mitaa inayohusu uchambuzi mfumo wa