banner

Pangani

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


 

  • Wilaya ya Pangani ni mojawapo ya Wilaya zinazounda Mkoa wa Tanga. Wilaya hii ilianzishwa enzi za Ukoloni wa Kiingereza  na ni mojawapo ya Wilaya ya Zamani sana hapa nchini.

      1. MIPAKA YA ENEO

    Wilaya ya Pangani iko kusini mwa Mkoa wa Tanga, upande wa Kaskazini inapakana na Wilaya ya Muheza ambapo Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi. Kwa upande wa Magharibi Pangani inapakana na Wilaya ya Handeni wakati kusini ipo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Mji wake Mkuu unaitwa Pangani na uko kilomita 50 toka makao makuu ya Mkoa wa Tanga. Eneo la Wilaya ni Kilomita za Mraba 1,830.8 zinayoifanya kuwa Wilaya ndogo kuliko zote Mkoa wa Tanga


  • View Larger Map

Idadi ya Watu na namna wanavyoongezeka
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002 Wilaya ilikuwa na  watu 44,107 kati yao wanaume ni 22,224 na wanawake 21,883 zipo kaya 11,283 zenye wastani watu 3.9 kila kaya. Kwa  mwaka 2011 Wilaya inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 46,078.

2.2.1  Mgawanyo wa watu
Asilimia 85 ya wakaazi wanaishi vijijini na asilimia 15 wanaishi maeneo ya Mjini. Makabila yaliyopo Wilayani ni Zigua, Bondei, Sambaa, Pare na Wamasai.