banner

Tanga

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Halmashauri ya Jiji la Tanga ni moja kati ya Halmashauri tisa za Mkoa wa Tanga. Nyingine ni Pangani, Mkinga, Muheza, Korogwe mji, Korogwe wilaya, Lushoto, Handeni na Kilindi. Ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 600 kati ya hizo kilomita za mraba 62 ni eneo la maji (covered with wáter bodies). Halmashauri ya jiji la tanga ipo kati ya 38053’ na 39010’mashariki, na 50 na 5016’kusini, kaskazini mashariki mwa Tanzania. Eneo kubwa ni tambarare na maeneo machache ni miinuko midogomidogo.

 

Idadi ya watu
Kwa mujibu wa  sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, jiji la Tanga lilikuwa na jumla ya idadi ya watu 242,640 ambao ni karibu asilimia 14.8 ya watu wote wa mkoa wa tanga. Kati ya hao 119,621 walikuwa wanaume (49.3%) na watu 123,019 walikuwa wanawake (50.7%) karibu asilimia 37.5 ya watu wote walikuwa watoto chini ya miaka 15 na watu wenye uwezo wa kufanya kazi (potential labour forcé) walikuwa ni asilimia 58.8 ya watu wote ambao walikuwa watu wenye umri kati ya miaka 15-64. Wastani wa watu kwenye kaya ilikuwa ni karibu watu 4.6 na mtawanyiko wa watu(population density) ulikuwa ni wastani wa watu 451 kwenye eneo la kilomita ya mraba . kutokana na ongezeko la watu la asilimia 1.88 kwa mwaka(population growth rate) jiji la Tanga kwasasa linakadiriwa kuwa na watu 292890

Hali ya hewa
Hali ya hewa ni ya ukanda wa pwani ambao una joto la wastani ya sentigredi 240C mpaka 330C. Tanga inapata mvua ya misimu mitatu kama ifuatavyo:-

  • Mvua ndefu za masika ambazo zinaanza katikati ya mwezi wa Machi mpaka Mei  kwa kiasi cha milimita 1000 mpaka 1,400 
  • Mvua nyepesi za mchoo ambazo zinanyesha kati ya mwezi wa julai mpaka augosti kwa kiasi cha milimita 100
  • Mvua fupi za vuli zinazonyesha kati ya mwezi oktoba na Desemba kwa kiwango cha milimita 500 mpaka 800

Uoto wa Asili
Uoto wa asili wa halmashauri ni vichaka na misitu ya asili.  Misitu ya mikoko katika ukanda wa pwani yenye ukubwa wa hekta 1,200 mpaka 3,000. Misitu ya asili ni hekta 1,500 na sehemu iliyobaki ni mimea iliyopandwa na watu.