WAKAZI wa Jiji la Tanga wamejitokeza kushiriki na kushuhudia Tamasha la Chapati lililofanyika eneo la Forodhani, likilenga kuenzi utamaduni wa vyakula vya asili, kukuza ubunifu na kuhamasisha mshikamano wa kijamii.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe.l Balozi DktbBatilda Burian, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo jana, ameridhishwa na mwitikio wa wananchi na ubunifu uliodhihirishwa na washiriki mbalimbali, wakiwemo wajasiriamali wa chakula na sanaa.
“Tamasha hili ni ishara ya mshikamano, amani, na upendo miongoni mwa wakazi wa Tanga. Ni jukwaa muhimu la kuenzi utamaduni wetu, lakini pia lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja,” alisema Mhe Balozi Dkt Batilda.
Mhe Balozi Dkt Batilda aliwapongeza washiriki wa tamasha hilo na wananchi waliohudhuria, kwa nidhamu na amani waliyoonesha wakati wote wa tamasha.
Alisema matukio kama tamasha hilo ni miongoni mwa ishara chanya za utulivu wa kijamii, hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Mhe.Balozi Dkt Batilda amewahimiza wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kupiga kura, akisisitiza kuwa kuchagua viongozi bora ni msingi wa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.