Serikali Mkoani Tanga imesema itaendelea kuhakikisha inaboresha na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi kwa manufaa ya mkoa na Nchi kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda mbalimbali vikivyopo mkoani humo.
Kindamba amesema nia ya serikali ni kuona wawekezajj wanafanya shughuli zao pasipo kuwa na vikwazo lakini pia wananchi wananufaika na uwepo viwanda hivyo kwa kupata ajira.
"Nia ya Serikali ni kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kufanya shughuli zao bila ya usumbufu huku wakiendelea kulipa kodi kwa hiari na watu wetu kupata fursa za kuajiriwa" amesema Kindamba
Aidha Mkuu wa mkoa amesema kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali kwa wawekezaji kwa mwaka 2022 wawekezaji waliweza kuchangia kwa kulipa kodi na tozo kwa serikali takribani shilingi Bilioni 12.
"Nimepitia ripoti zao mwaka jana tu ukichukua tozo mbalimbali na kodi za serikali wamechangia uchumi wa nchi yetu karibu Bilioni 12 huku wakitoa ajira za wastani takribani watu 1200" aliongeza Kindamba.
Pia Mhe. Kindamba amewatoa hofu wawekezaji hasa wa viwanda kuhusu suala la umeme na kuahidi kuwa mpaka kufikia Julai Mosi tatizo la umeme mkoani Tanga itakuwa Historia.
Nae msaidizi mkuu idara ya fedha idara kiwanda cha kuzalisha saruji cha Maweni limestone Peter Shuma amesema kuwa maboresho ya bandari ya Tanga yamesaidia kurahisisha shughuli za usafiri wa saruji kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa urahisi.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.