• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

SPIKA WA BWZ ASEMA, UKUBWA WA MIRADI YA MAENDELEO NI ISHARA YA UBORA WA RAIS SAMIA

Imewekwa tarehe: April 24th, 2025

Na Mashaka Mgeta,  HANDENI

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BWZ), Mhe Zubeir Ali Maulid, amesema miradi mikubwa inayotekelezwa kupitia sekta mbalimbali nchini, ni miongoni mwa ishara kuu za ubora wa uongozi wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mhe Maulid ameyasema hayo leo Aprili 24, 2025 baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi maabara ya Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Mji Handeni ambayo ni sehemu mradi uliogharimu Shilingi milioni 900.

Mhe Maulid yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Tanga,  ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofikiwa Aprili 26, 1964 na ‘kuizaa’Tanzania.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake, Mhe Rais Dkt Samia ametekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakiwemo maboresho wa miundombinu na ujenzi wa maabara kwenye hospitali hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju amesema, mwaka 2023/2024, halmashauri hiyo ilipokea Shilingi milioni 900. Kati ya fedha hizo, Shilingi milioni 250 zilitumika kwa ujenzi wa maabara na Shilingi milioni 400 kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU).

Pia, Shilingi milioni 111 zilitumika kwa ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti, Shilingi milioni 44,000,000 kwa ujenzi wa njia na Shilingi milioni 95 kwa ukarabati wa miundombinu chakavu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na Mganga Mkuu wa Handeni Mji, Dk Hudi Shehdadi, ujenzi wa maabara hiyo uliofikia asilimia 81, ulianza Juni 14, 2024 na unatarajiwa kukamilika Mei 28, mwaka huu.

Amesema, maabara hiyo itahifadhi damu salama hivyo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto chini ya miaka mitano na kuongeza wigo na ufanisi katika kutoa huduma za kiuchunguzi wa magonjwa ya binadamu

Faida nyingine ni kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaohitaji vipimo vikubwa vya kimaabara kama vile uoteshaji wa vimelea vinavyosababisha usugu wa maradhi ya kuambukiza,  ambao kwa sasa vinasafirishwa hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga iliyopo umbali wa  kilomita 160 kutoka Handeni.

 

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MZUMBE KUKUZA UJUZI UNAOKIDHI RASILIMALI ZA KIUCHUMI

    February 16, 2026
  • MWIGULU ASEMA: NINASAFISHA 'VICHAKA VYA UBADHIRIFU' WA MALI ZA UMMA

    February 15, 2026
  • AWESO, MHANDO WAPIGA MAGOTI KUOMBA BARABARA YA LAMI TANGA

    February 15, 2026
  • AWESO, MHANDO WAPIGA MAGOTI KUOMBA BARABARA YA LAMI TANGA

    February 15, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.