Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe Mohamed Mchengerwa, atakutana na Maafisa Mawasiliano wa Sekretarieti za Mikoa na Maafisa Habari wa Halmashauri nchini Mei 23 na 24, mwaka huu.
Kikao hicho cha mafundo na mazingativu, kitafanyika jijini Dodoma, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kiutendaji kwa maafisa hao.
Taarifa ya TAMISEMI imeeleza, kupitia kikao hicho, utawekwa mkakati endelevu wa kuhabarisha umma kuhusu hatua mbalimbali za maendeleo ya nchi, hususani katika uongozi wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Maafisa hao wamekuwa kiunganishi bora kati ya wananchi na Serikali, na kupasha habari za Serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu yake.
Pia taarifa hiyo ya TAMISEMI imesema Maafisa Mawasiliano na Habari wa Serikali, wamefanikisha kuuhabarisha umma kuhusu mafanikio na changamoto na kupaza sauti za wananchi.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema, amesema kikao hicho kwa kada hiyo ni muhimu sana hasa kwa wakati huu kunapohitajika nguvu za kuboresha na kuimarisha zaid mawasiliano na kati ya Serikali na wananchi.
Mnyema ameshawaelekeza Wakurugenzi wa halmashauri 11 za mkoni humo, kuwawezesha Maafisa Habari wao kushiriki kikao hicho kwa ufanisi.
”Sisi (Tanga) hatuna mzaha katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali, tunatambua umuhimu wa kikao hiki na mwaliko wa Mhe Waziri ni maelekezo, hivyo kila halmashauri itamuwezesha Afisa Habari wake kushiriki,” amesema.
Maafisa Habari wa mkoani humo, wameelezea kupata muitikio mzuri wa Wakurugenzi wao, na wana imani ushiriki katika kikao kazi hicho utaongeza chachu yenye kuleta matokeo chanya katika utendaji kazi wao, halmashauri na mkoa wa Tanga.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.