• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

WAJASIRIAMALI TANGA ‘WAMVULIA KOFIA’ RC BALOZI BATILDA

Imewekwa tarehe: July 9th, 2024

Na Mashaka Mgeta, DAR ES SALAAM

 

ILE kauli mbiu ya ‘Tanga Lango Kuu la Uchumi Afrika Mashariki’ inazidi kutanua wigo wa maendeleo ya wakazi wa mkoa huo, kutokana na hatua mbalimbali ikiwemo ushiriki wa wafanyabiashara na wajasiriamali wake kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.

 

Wafabiashara na wajasiriamali hao wanaofikia 17, wanasema ubunifu, ushirikishaji na maelekezo ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe Balozi Batilda Burian, kuwagharamia kushiriki maonesho hayo yenye hadhi kubwa ya kufungua na kuongeza fursa za kiuchumi, haijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita.

 

Baada ya kuwasili mkoani Tanga Machi 13, 2024 kufuatia kuhamishiwa kutokea mkoani Tabora Machi 9, 2024, Mhe Balozi Dk Batilda akasema miongoni mwa njia za kuipa maana kubwa kauli mbiu ya ‘’Tanga Lango Kuu la Biashara Afrika Mashariki’’ ni pamoja na kuwapa fursa wafanyabiashara na wajasiriamali mkoani humu, ni kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali wenyeji kushiriki maonesho hayo.

 

Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wa Tanga, Pili Mnyema, amewatembelea wafanyabiashara na wajasiriamali hao jana Julai 7, 2024, akazungumza nao na kuwahakikishia nia ya Serikali ya Mhe Rais Dk Samia Suluhu, kukuza na kuwajengea uwezo zaidi wa kumudu ushindani kwenye soko.

 

Siri Sadik maarufu kama Binti Sadi, mjasiriamali wa Pangani anayetengeneza bidhaa za asili  kwa matumizi mbalimbali, zikitokana na malighafi zinazopatikana mkoani Tanga, anasema ingawa hii ni mara ya 12 kushiriki maonesho hayo, lakini mwaka huu, asingeshiriki kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, hadi alipojulishwa kuhusu mwaliko wa Mhe Balozi Batilda kwao.

 

‘’Mwaka huu sikuwa na wazo la kuja Sabasaba kutokana na hali ya kifedha kutokuwa nzuri, lakini Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga, na kupitia jitihada za Mhe Balozi Batilda, nimeweza kushiriki, tena kwa namna ambayo haijawahi kutokea, kwa maana tofauti na wakati mwingine, safari hii tunatambulika rasmi kwenye banda la mkoa wa Tanga,’’ anasema.

 

Mjasiriamali anayesifika zaidi kwa biashara ya unga bora wa mwani, Hajra Ali, anasema ushiriki wake wa mara kwanza kwenye maonesho hayo, umemfungua ufahamu zaidi wa kutambua namna tofauti za uzalishaji, usindikaji na kutafuta masoko, hivyo kumuongezea ujuzi, mbinu na stadi kwenye biashara zake.

 

‘’Ingawa kwa upande wa mauzo naona yapo chini kuliko nilivyotarajia, lakini nimepata mbinu, stadi na ujuzi mkubwa sana wa namna ya kushiriki na kukuza biashara zangu,’’anasema.

 

Mjasiriamali Grace Anania anasema, kabla ya kujiunga na kampuni ya Enika Collections inayotengeneza bidhaa zinazotumia zaidi nyuzi za katani, alikuwa hajaelewa manufaa ya ujasiriamali huo, lakini sasa anafikiria kukua zaidi kupitia uzoefu na kujifunza kutoka kwa washiriki wengine wa maonesho hayo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TANGA 'YAITIKA' WAZIRI MCHENGERWA AKIWAITA MAAFISA HABARI WA MIKOA, HALMASHAURI DODOMA

    May 21, 2025
  • KATIBU MKUU IKULU AFUNGUKA NA KUWAELEKEZA WATUMISHI WASIKIUKE MAADILI

    May 20, 2025
  • WATUMISHI WAELEKEZWA, JENGENI DESTURI YA KUZISOMA SHERIA NA KANUNI

    May 19, 2025
  • HISTORIA YA UKOSEFU WA MAJI INAFUTWA MUHEZA

    May 19, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.