Na Emma Kigombe |
Watahiniwa wapatao 65, 955 wameanza mitihani yao ya kuhitimu Elimu ya msingi katika mkoa wa Tanga ambapo kati ya waliosajiliwa wavulana ni 30,831 na wasichana 35,145.
Jumla ya Shule zilizosajikiwa ni 1057 ambapo shule za Serikali ni 996 na binafsi ni 61 katika Halmashauri zote 11 za mkoa wa Tanga.
Akizungumza Afisa Elimu wa mkoa wa Tanga Newaho Mkisi amesema mkoa wa Tanga umejipanga vizuri kuhakikisha mitihani inafanyika pasipo kikwazo chochote.
Newaho amewataka wote wanaohusika na usimamizi wa mitihani hiyo kufanya kazi kwa bidii huku wakizingatia uwaninifu na kuepuka vitendo vitakavyoweza kuharibu mitihani hiyo.
"Waalimu tutakaohusika na kazi hii maalumu nawakumbusha tufanye kazi kwa bidii na umakini mkubwa tukizingatia uadilifu huku tukijiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuharibu mitihani kwa kuwa Serikali haitafumbia macho kwa mtu yoyote atakayefanya udanganyifu au kuharibu zoezi zima la mitihani" alisema afisa Elimu
Sambamba na hilo amewataka wanafunzi kutulia na kujiamini kwa kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha kufanya mtihani huo.
"Kwa miaka saba tumeshajifunza mengi, tumeweza kukamikisha mada, tumefanya mazoezi ya kutosha ninaamini kupitia mitihani iliyokuwa inafanyika mara kwa mara watafanya vizuri na kufahulu" aliongeza afisa Elimu.
Mitihani ya kuhitimu Elimu ya msingi inafanyika kwa siku mbili tarehe 13 na 14 nchini kote.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.